Wanafunzi wa kigeni kupungua Uingereza!!


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Alan Johnson, amesema kuwa serikali itapunguza idadi ya hati za kuingilia nchini humo au visa kwa wanafunzi wa kigeni ikiwa ni hatua inayolenga kukomesha utumiaji vibaya wa mfumo huo.
Bw Johnson alisema sheria kali zitawalazimisha watu wanaomba visa wawe wanakimudu Kiingereza katika kiwango fulani.
Pia watu ambao wanahudhuria kozi za muda mfupi nchini Uingereza, hawatoruhusiwa kuwaleta jamaa zao kama vile mke au watoto.
Waziri Johnson aliongeza kuwa sheria hizi haziwalengi wanafunzi wenye nia ya kweli ya kusoma, bali wale ambao lengo lao halisi lilikuwa ni kufanya kasi nchini Uingereza.
Kanuni hizi mpya zinafuatia amri ya kutathmini upya sheria za uhamiaji iliyotolewa baada ya jaribio la kulipua ndege ya Marekani, mwezi December mwaka uliopita.
Uamuzi huo ulitolewa na Waziri Mkuu, Gordon Brown, baada ya kusema kuwa mshukiwa aliyetaka kulipua ndege hiyo,Umar Farouk Abdulmutallab, ambaye alisomea mjini London, alijiunga na al-Qaeda nchini Yemen baada ya kuondoka Uingereza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment