ONYESHO LA "LADY IN RED" NI ZAIDI YA UBUNIFU WA MAVAZI, LACHANGISHA FEDHA KITUO CHA YATIMA CHA (TMH)

Farha Mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka 2010 akipozi kwa picha mara baada ya kupokea zawadi yake ya maua na cheti kutoka kwa mkurugenzi wa Fabak Fashion Asia Idarous kwenye onyesho kubwa la mavazi linalojulikana kama Lady In Red lililofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana usiku na kuhusisha wabunifu mbalimbali wakiwemo chipukizi na wakongwe, katika onyesho hilo zilionyeshwa nguo za wabunifu mbalimbali na kulifanyika mnada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuchangia watoto katika kituo cha watoto yatima cha Tanzania Mitindo House (TMH) kinachosimamiwa na wanamitindo mbalimbali wakiongozwa na mbunifu Khadija Mwanamboka na kutolewa ahadi mbalimbali za kiasi cha shilingi 500.000.
Katika onyesho hilo burudani zilitolewa na bendi ya Machozi na kundi la ngoma za asili la Simba Thietre kutoka jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Asia Idarous na kushoto ni mwakilishi wa kampuni ya Dalling iliyodamini onyesho hilo, mdau hebu angalia katika picha hizi uone jinsi wanamitindo walivyoonyesha mavazi jukwaani






You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment