Moja kati ya matukio wakati klabu za Simba na Manyema zote za Dar es Salaam zilipopambana na Simba kuifunga Manyema 2-0.
Magoli ya timu ya Simba ya jijini Dar es salaam yaliyofungwa na wachezaji wake Ulimboka Mwakingwe na Mussa Hassan Mgosi yalitosha kabisa kuizamisha timu ya Manyema Rangers ya jijini Dar es salaam pia kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Katika Mchezo huo uliokuwa na upinzani katika kipindi cha kwanza uliichukua timu ya simba muda mrefu mpaka kufanikiwa kupenya ngome ya timu ya Manyema na kufanikiwa kupata goli la kwanza kwenye dakika ya 63 ya mchezo huo kwa goli safi lililofungwa na Ulimboka Mwakingwe.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa timu ya Manyema aka "Mkuki wa Sumu" baada ya kuwachezea vibaya Mussa Mgosi katika eneo la hatari hivyo kusababisha adhabu ya Penati katika lango lao na kumfanya mchezaji huyohuyo Mussa Mgosi kufunga goli katika dakika ya 71.
Kwa matokeo hayo ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manyema Rengars ina maana timu ya Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi 46 ikiwa ni tofauti ya poiti 10 dhidi ya watani wao Yanga wanaofuatia kwa pointi 36.
0 comments:
Post a Comment