Bunge la Senate nchini Nigeria, kutokana na rais Umaru Yar'Adua kuugua kwa muda sasa, limepiga kura na kuamua kumkabidhi madaraka makamu wa rais.
Katika mjadala mkali bungeni, maseneta hao walisema hatua hiyo ilibidi ili kuiepusha nchi hiyo kwa kukosa uongozi thabiti, na kuwepo pengo katika uongozi, jambo ambalo linazuia maendeleo.
Pengo hilo la uongozi limekuwepo nchini Nigeria tangu mwezi Novemba mwaka jana, wakati Umaru Yar'Adua alielekea Saudi Arabia kupata matibabu.
Waandishi wa habari wanaelezea kwamba bado haijafahamika wazi ikiwa kura ya bunge ina uwezo kamili katika kumkabidhi uongozi makamu wa rais, Goodluck Jonathan.
Bunge dogo la Nigeria, leo pia linajadili tatizo hilo la uongozi.

0 comments:
Post a Comment