Commercial Bank of Africa CBA yapata faida ya bilioni 2.5 mwaka 2009!!


Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Commercial Bank of Africa CBA Nehemiah K. Mchechu akizungumza na waandishi wa habari
kutoka Kushoto mkuu wa kitengo cha wateja binafsi benki ya CBA David Shambwe, Rashid Tenga Mkurugenzi wa kampuni ya Aggrey & Clifford na Stanlry Kafu mkuu wa Uhasibu kampuni ya Aggery & Clifford.
Commercial Bank of Africa CBA leo imetangaza kupata faida nono ya bilioni 2.5 kwa mwaka 2009 na kuonyesha kuwa ni benki imara inayojitoshereza kwa kuwa na mtaji wa kutosha,Pamoja na mtikisiko wa dunia kiuchumi uliozikumba taasisi nyingi za fedha mwaka uliopita, benki hii imeendelea kukua na kujiimarisha.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja, mtaji wa CBA umekuwa kwa bilioni Tshs 57, au aslilimia 56, kutokana ongezeko la asilimia 67 la amana za wateja, kutoka Tshs 35 bilioni na kuwa Tshs 87.5 bilioni. Mafanikio haya ni matunda ya bidii, busara na mikakati madhubuti ya CBA.
Moja ya mikakati hiyo imekuwa ni kuweka kiasi cha mtaji wa Tshs 3.2 bilioni mwaka 2009 ili kusaidia mpango wake wa kukua na kupanuka,
Matokeo hayo kwa hakika yamekuwa ni ya kufurahisha na Msimamo wa muda mrefu wa benki, uwezo wa kubaini matatizo na kuchukua tahadhari mapema, uzingatiaji wa kanuni bora za kibenki, mtaji imara, sera za muda mrefu za kukopesha, na uwekezaji kwenye huduma kwa wateja vimevutia wanahisa ambao wamewezesha kuwa na ongezeko la kifedha kutoka Tshs 7.3 bilioni mpaka Tshs 14 bilioni.
Mafanikio hayaishii hapo tu Kwani lengo ni kuwa na wateja wengi na kuwafikia kwa urahisi zaidi, CBA hivi karibuni imefungua tawi jipya huko Mbeya na iko mbioni kufungua matawi mengine mapya manne; Kariakoo, Ohio Street (Dar es Salaam), Mwanza na Arusha.
Makao makuu ya CBA pia yanahamia mtaa wa Ohio kwenye tawi jipa lilipo jengo jipya la Amani Place. Tawi linatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo Februari 15, 2010.
“CBA iko mstari wa mbele katika kutoa huduma bora kwa wateja wake wanaoongezeka kila siku na inatarajia kuzindua bidhaa mpya na utaratibu mpya wa kibenki ili kuendana na mahitaji ya wateja wake" amesema Nehemiah Mchechu, Mtendaji Mkuu wa CBA, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kwa kuzingatia mkakati wake wa kuwa taasisi inayoongoza kwa kutoa huduma nzuri za kifedha, CBA inamalengo maalum ya kimasoko kwa wateja wadogo wadogo na wakubwa na imeungana na Umoja SWITCH ATM ambao wako katika hatua za mwisho za kusambaza kadi za ATM.
Kumekuwa na mwitikio wa ajabu. – mikopo imepanda kufikia asilimia 57, au Tshs 22 bilioni, kutoka 2008. mahitaji ya kukopesha yaenda sambamba na ukuaji wa mapato; mapato yanayotokana na riba yamepanda kwa asilimia 58 kutoka Tshs 6.7 bilioni kama ilivyoonyeshwa kwenye vitabu vya mwaka 2008 hadi Tshs 10.7 bilioni kwa kipindi kilichoishia 31 Desemba 2009.Kwa ujumla, haya ni mafanikio ya kuridhisha kwa benki ambayo imeendelea kuimarika kutokana mafanikio ya kipindi kilichopita. Kuanzia 2007 ambapo faida isiyolipiwa ushuru ilikuwa Tshs 215 milioni, 2008 Tshs 1.4 bilioni, 2009 Tshs 2.5 billioni, CBA iko katika nafasi nzuri ya kuhimili mikikimikiki ya kifedha inayoweza kutokea.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment