MICHUANO YA KICKBOXING KUFANYIKA MWEZI HUU!!

Mchezaji wa mchezo wa Kickboxer na mkurugenzi wa kampuni ya Tan Academy of Mix Fight & Thai Boxing Japhet Kaseba akionyesha picha wakati akizungumzia Ligi ya Bingwa wa Mabingwa wa mchezo wa Kick Boxing Tanzania itakayofanyika kwenye ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa jijini Dar es salaam inayotarajiwa kuanza tarehe 27 mwezi wa pili na kuisha tarehe 27 mwezi wa tatu mwaka huu, ligi hii itakutanisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali, lakini changamoto kubwa katika michezo hiyo ni mabondia wanawake Upendo Njau kutoka kirimanjaro na Frola Machela kutoka Dodoma ambao watapambana katika michezo hiyo,
Michezo hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka ili kutafuta washindi ambao hapo baadae wakauwa na uwezo wa kuingia kwenye mashindano ya kamataifa ili kuongeza ari na kukuza zaidi mchezo huo hapa nchini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment