BENDI ya muziki wa dansi ya K-Mondo Sound ya mjini Dar es Salaam inatarajiwa kufanya onyesho la siku ya wapendanao katika hoteli ya Picolo Beach, Dar es Salaam ikisindikizwa na onyesho la Mavazi. Meneja wa bendi hiyo, Aunt Connie Karanja ameiambia Dimba kuwa katika onyesho hilo ambalo kiingilio kitakuwa sh 50,000 kwa VIP na 30,000 kwa viti vya kawaida, kutakuwa na mavazi maalum ya Valentine. “Bendi yetu itafanya onyesho hapo pamoja na Mariam Kamegisha wa Uganda wengi wanamfahamu kama Tinatine, lakini pia kutakuwa na onyesho maalum la mavazi ya valentine,” alisema. Alisema mbunifu wa kitanzania, Dina Designer ataonyesha nguo zake mpya ambazo zitajumuisha matukio mbalimbali. K-Mondo inatamba na nyimbo zake za Magambo, Sharufa, Njiwa, pamoja na ule wa Tatizo Umasikini ambao umeimbwa na Vumi Mwaipopo. Nyota wengine wanaounda kundi hilo ni pamoja na Richard Mangustino ambaye ni mwimbaji na mtunzi pamoja na Mhina Panduka ‘Toto Tundu’.
Fashion Shoo kusindikiza K-Mondo Valentine!!
Posted by
ADMIN
Kiongozi wa K. Mondo Sound Mangustino.
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment