Mjumbe wa kudumu wa CAF mwanasheria Said El Maamri amesema shirikisho la mpira wa miguu la CAF halikukosea kuifungia timu ya taifa ya Togo mara baada ya kujitoa kwenye michuano ya kombe la Mataifa huru ya Afrika yaliyomalizika hivi karibuni nchini Angola.
El maamri ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo wakati akifafanua mambo mbalimbali kutokana na hatua ya shirikishom la mpira wa miguu la CAF kuifungia Togo.
Amesema Serikali ya Togo iliingilia masuala ya mpira wakati kanuni na sheria za FIFA na CAF zinasema mambo ya mpira yasiingiliwe na serikali za nchi husika badala yake viachiwe vyama vya mpira vya nchi hizo vishughulikie mpira.
Ameongeza kuwa kimsingi kwa kanuni za CAF timu zote zilizokuwa zikienda Angola kwa ajili ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika zilitakiwa kutumia usafiri wa ndege ili kufika huko, lakini Togo walichukua ndege kutoka Lome Togo na kutua katika mji wa PortNoer nchini Congo Brazzavile, baada ya kufika hapo waliamua kutumia usafiri wa basi, hata hivyo walitoa taarifa ya kutumia usafiri wa basi katika muda mfupi sana na kupewa ulinzi wa magari mawili na askari kabla ya kuelekea jimbo la Cabinda ambako ndiyo kilikuwa kituo chao cha mashindano , walipokuwa njiani katika msitu ndipo waliposhambuliwa na waasi ambao wanapambana na chama cha MPLA kinachatawala nchini Angola.
Katika shambulio hilo baadhi ya watu walipoteza maisha akiwemo kocha msaidizi wa timu hiyo huku wengine wakijeruhiwa.
Kutokana na tukio hilo Mwenyekiti wa CAF Issa Hayatou na baadhi ya wajumbe wa CAF kutoka kituo cha Luanda walienda Cabinda na kukutana na uongozi wa Timu ya Togo na wachezaji ambapo CAF iliipa Togo maagizo mawili ili waone ni kipi kitafaa kwao na waseme iwapo wataendelea na mashindano au hawataendelea na mashindano na jibu lolote ambalo wangelitoa CAF ingekubaliana nao, Viongozi na wachezaji wa Togo walikubali kuendelea na mashindano
.Hata hivyo Serikali ya Togo iliwaamuru wachezaji wake kurejea nyumbani na kwamba mchezaji yeyote ambaye angebaki Angola angekuwa amepoteza uraia wake wa Togo, hivyo wachezaji pamoja na viongozi wao walitii agizo la serikali yao na kurejea Togo.
Kutokana na mkanganyiko huo tayari serikali ya Togo ilikuwa imeingilia masuala ya michezo kitu ambacho sheria na kanuni za shirikisho la mpira wa miguu la FIFA na CAF zinakataza serikali kuigilia masuala ya michezo.
Katika suala hili ilitakiwa Serikali ya Togo iwasiliane na Serilaki ya ya Agola kuhusu masuala ya usalama wa wachezaji kama waliona kulikuwa na wasiwasi zaidi juu ya hilo na walitakiwa kuliachia shirikisho la mpira la Togo kuwasiliana na CAF ili kushughulikia suala la timu ya Togo kurejea nyumbani au kubaki na siyo Serikali kwa kuwa CAF inawasiliana na shirikisho la soka la Togo na siyo Serikali ya Togo.
0 comments:
Post a Comment