Daladala aina ya Toyota DCM liliogonga kichwa cha Treni maeneo ya Tandika Relini na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye inadaiwa kuwa ni dereva na kujeruhi wengine 26 waliokimbizwa hospitali ya Temeke kwa matibabu hata hivyo wagonjwa 5 kati ya hao walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya sana kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata katika ajali hiyo.
Wakazi wa eneo la Tandika Relini wakiwakielekea kwenye eneo la ajali iliyotokea leo majira ya saa tano asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na na kujeruhi wengine 26.
1 comments:
Kaka,
Nawapa pole maalumu wafiwa na majeruhi! Pole zaidi kwa waTanzania kwa maelfu ambao kila siku wanapanda madaladala.Au tuyaite machakavu?!
Hii nchi sijui vipi kwa kweli? Nashindwa kugundua cancer yake iko wapi au anaineemesha nani!
Kwa wale madereva wenzangu, mnafahamu "uendeshaji wa kigaidi" unaofanywa na madereva wa haswa aina hilo la gari, DCM!
Kwa wale mnaopita njia ya Airport, kuna yale yenye logo za kiNazi! Aisee!!
Mimi mnyonge wa Kawawa Road ndio usiseme! Bora wenzetu huko Ali Hassan Mwinyi, sijui vipi hamna maDCM? Aaaaah, kielelezo cha ubora wa matabakaaaaaaaa!! Mungu ee!
Wanachomekea kiholela, wanafukuzana hovyo kama watoto vile, wanaziba njia, wanaweza hata kukutoa barabarani kwa kupita sambamba katika njia moja! Yaani ni uhuni na vurugu tupu!! Foleni ZOTE jijini hutokana na daladala wala sio kitu kingine!!
Hayo makweche hayana thamani, likigonga au wakingongana, chapchap linaenda kuungwa au kunyooshwa, saa moja baadaye wanatafutana ubaya!!
Tukiamua kufuatilia hilo kweche hapo, nahakika next week litakuwa road tena.
Nani anayakagua haya magari, nani anaweza simamia nidhamu na huduma bora kwa abiria, HAKUNA!
Kwa kweli, ningepata cheo fulani cha uendeshaji jiji hili, ningemeza vidonge vya kupunguza maumivu ya kuchukiwa lakini ningesababisha nidhamu, usafi na maendeleo ya ustawi wa jamii katika jiji ambalo hata mfumo wa usafiri ni kichaa tupu!!!
Inaboa kweli!!
Taji
Post a Comment