SERENGETI YAKANUSHA HABARI ZILIZOANDIKWA KWENYE GAZETI LA NEW VISION (UGANDA)

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira Tanzania TFF Fredrick Mwakalebela akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya kiwanda cha bia cha Serengeti Chang'ombe Temeke jijini Dar es salaam, anayefuatia katika picha ni Meneja uhusiano wa kamuni hiyo Teddy Mapunda na mwisho ni Msemaji wa TFF Frolian Kaijage.

Gazeti la New Vision la Uganda toleo la Januari 6/ 2010 lilichapisha habari likieleza kuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti ndiyo iliyokataa maombi ya Uganda ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Coast wakati timu hiyo ilipokuwa Tanzania kujiandaa na fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea huko nchini Angola. Gazeti hilo liliendelea kudai kuwa uamuzi wa Ivory Coast kucheza na Rwanda ulikuwa baadaye kwani Serengeti ilitaka Ivory Coast icheze michezo miwili na Taifa Stars kwa madai kuwa Serengeti ilitaka kurejesha fedha ambazo ziliwekezwa kwenye ziara hiyo.

Habari hiyo ambayo kwa hakika haina ukweli wa aina yoyote ilimnukuu afisa wa Shirikisho la mpira wa miguu la Uganda FUFA aitwaye Moses Magogo akitoa madai hayo. Hata hiyo habari haikueleza Magogo ana cheo gani ndani ya FUFA.Serengeti Breweries inapenda kuufahamisha umma kuwa majukumu yake katika mpira yanafahamika vizuri kulingana na Mkataba ambao inao na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

Kazi ya SBL ni kutoa fedha kwa ajili ya kulipia gharama kama zilivyoainishwa kimkataba.Si kazi ya SBL kualika timu za kucheza wala kuamua ni timu gani icheze na Taifa Stars au timu nyingie yoyote ile. Hiyo ni kazi ya TFF.Kwa mantiki hiyo tunapenda kuufahamisha umma kuwa habari nzima iliyoadikwa na gazeti hilo ni ya uongo na haina chembe ya ukweli.

Hata hivyo SBL inafahamu vema kwamba Uganda kupitia FUFA walialikwa na TFF na walijibu kwa maandishi kuwa hawawezi kuleta timu yao kwa sababu wanazozijua. Sasa hatuelewi maneno mengine yanatoka wapi. Ni wakati wa kupuuza uzushi wa namna hii wenye lengo la kuleta mtafuruku na kuvuruga uhusiano baina ya vyama vya mpira na wadhamini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment