Dar es Salaam, Januari 14.2010. Vodacom Tanzania imezindua awamu ya pili ya Promosheni yake kubwa ya Tuzo millionea ambayo itamuwezesha mteja mmoja wa Vodacom kushinda Sh. Milioni 100 taslim na wengine wengi kushinda zawadi kemkem.
Droo kubwa itafanyika mwezi Aprili mwaka huu.Mbali na mshinndi huyo pia wateja watapata nafasi ya kujishindia muda wa maongezi wenye thamani ya Sh. Milioni tisa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, alisema kupitia promesheni huyo, wateja saba wa Vodacom watajishindia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 100,000 kupitia droo za kila wiki.
Droo zitafanyika kwa wiki 12 kuanzia sasa na hivyo wateja kujipatia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni tisa.
Rwehumbiza alisema promosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Tuzo milionea iliyoendeshwa na kampuni hiyo mwaka jana.
Mshindi wa Droo kubwa ya mwaka jana alikuwa ni Renatus Mkinga, Mkazi wa Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam, Mkinga alishinda shilingi milioni 100 na kuboresha maisha yake---alinunua gari na kujenga nyumba ya kisasa.
Aliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuanzisha promosheni hiyo ambayo alisema hakika inasaidia kubadili maisha ya Watanzania kama ilivyosaidia kubadili maisha yake ambayo sasa yataboreka.
Mkinga ambaye ni mstaafu, aliwataka Watanzania kushiriki katika promosheni hiyo na kuachana na propaganda za kwamba washindi huwa wanapangwa.
“Tuache imani hizo potofu, mimi nimeshiriki mara nyingi katika promsheni hii na hatimaye Mungu akanisaidia nikawa mshindi, hivyo tushiriki kwa wingi ili tupate nafasi ya kushinda,” alisema wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi yake ya fedha taslim Aprili mwaka jana,”
Rwehumbiza alisema promosheni hiyo ni kwa wateja wa akaunti za malipo ya kabla na baada.
Alifafanua kwamba mbali na droo za kila wiki pia kutakuwa na droo kubwa za kila mwezi ambazo zitawawezesha wateja wa Vodacom kushinda zawadi kem kem.
Ili kushiriki alisema mteja anajisajiri kwa kuandika neno milionea na kutuma kwenda namba 15588.
“Jinsi mteja anavyotuma mara nyingi ndivyo anavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda,” alisema.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom kuichangamkia promosheni hiyo kwani inalenga katika kuboresha maisha ya wateja wake.
“Promesheni hii inalenga kuboresha maisha ya wateja wetu lakini pia ni shukrani zetu za dhati kwa wateja wetu waaminifu kwa kutuwezesha kuwa mtandao unaoongoza Tanzania,” alibainisha.
0 comments:
Post a Comment