YANGA WAPIGA MARUFUKU UUZAJI WA VIFAA VYENYE NEMBO YAO!!

Msemaji wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam Bw. Louis Sendeu ametoa tamko kuwa klabu hiyo sasa imepiga marufuku na haitaruhusu mtu yeyote kutengeneza bidhaa zinazohusiana au zenye nembo ya klabu hiyo kwa lengo la kufanya biashara.
Sendeu ameyasema hayo wakati alipoongea na mwanablogu John Bukuku kutoka makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani, amesema kumekuwepo na uuzwaji holela wa vifaa kama fulana, skafu, jezi kalenda na vingine vingi vyenye nembo , lakini kalbu hiyo haifaidiki na chochote kinachouzwa na watu hao isipokuwa wanajinufaisha wao na maisha yao tu.
Amesema kwa sasa klabu hiyo inajipanga ili ianze kutengeneza yenyewe vifaa hivyo na kuviuza kwa manufaa ya timu ya Yanga ili kuongeza mapato ya timu yeo kwa ajili ya huduma mbalimbali za timu na wachezaji kwani fedha zitakazopatikana katika mauzo ya vifaa hivyo zitasaidia kuongeza mapato ya klabu.
Kumekuwepo na watu mbalimbali nchini kote ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya vifaa vinavyotengenezwa kwa kutumia nembo za vilabu vya ligi kuu hapa nchini hasa Simba na Yanga na kuviuza maeneo mbalimbali hasa wakati timu hizo zinapocheza na kujipatia fedha nyingi bila vilabu hivyo kufaidika na biashara ya vifaa hivyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment