Majak Daw
Mkimbizi kutoka Sudan ameandika historia kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kujiunga na ligi ya kulipwa ya mpira wa miguu ujulikanao kama Australian Rules.
Majak Daw mwenye umri wa miaka 18 amesajiliwa na mojawapo ya vilabu maarufu ya, North Melbourne.
Anatumai kuwa mafanikio yake yatawahamasisha Waafrika wengine waliohamia Australia kushiriki katika mchezo huo.
Majak Daw na familia yake walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan alipokuwa na umri wa miaka tisa na aliwasili nchini Australia mwaka 2003 baada ya kuishi nchini Misri.
Kijana huyo mrefu alianza kucheza Australian Rules Football miaka minne tu iliyopita.
Ubaguzi umemuandama Majak tangu ajiunge na ligi hiyo lakini anasema matusi anayotupiwa viwanjani yanamsaidia kumtia moyo zaidi.

0 comments:
Post a Comment