Kutoka kulia ni Wakurugenzi wa Clouds Entertainment Media Ruge Mutahaba na Joseph Kussaga wakiwa na wadau wengine wa burudani katika mazishi ya Dj Kim Abdulhakhim Magomelo yaliofanyika leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu, Kim alifariki jana jioni akisumbuliwa na matatizo ya ugonjwa moyo, pumu na homa ya matumbo Typhoid kwenye Hospitali ya Saint Monica iliyoko Manzese jijini Dar es salaam inayojishughulisha na kutibu magonjwa ya moyo na ameacha mke na watoto watatu.
Kim atakumbukwa na wapenda burudani kote nchini kwa mchango wake katika burudani alikuwa DJ mzuri na aliwahi kuandaa mashindano mengi ya kucheza Disco ambayo yaliwakutanisha wakali mbalimbali katika kucheza Disco wakiwemo akina Sammy Cool, Marehemu Black Mosses, Bob Rich na wengine wengi waliokuwa maarufu sana katika kucheza Disco zamani.
Kim Pia aliwahi kuandaa Bonanza lililokuwa likijulikana kama Rap Bonanza lililokutanisha vijana wengi katika muziki wa Kughani Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Abdulhakhim Magomelo AMEN.
Friends Of Simba hawakuwa nyuma kama unavyowaona hawa kulia ni C. Magori na Salim Try Again wakiwawakilisha wenzao.
1 comments:
pole kwa kunyuma ya taarifa. Masoud Masoud yupo tbc taifa siku hizi.
Post a Comment