Mkuu wa Mauzo wa Zantel Bw. John Mbaga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo leo wakati wa uzinduzi wa ofa mpya ya “MZUKA” ambayo itamuwezesha mteja wa Zantel kuongea kwa masaa 12 kwa Tsh 200 tu kuanzia saa nne na nusu usiku hadi saa nne na nusu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Bw. Fintan Lawler.
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imezindua ofa mpya inayoitwa MZUKA itayowawezesha wateja wake kupiga simu kwa masaa 12 kwa Tsh 200 tu kuanzia saa 4:30 usiku hadi saa 4:30 asubuhi kila siku.
Mkuu wa mauzo wa Zantel John Mbaga amesema kuwa Zantel ni kampunia ya kwanza kuwawezesha wateja wake kuongea kwa masaa 12 kwa Tsh 200 tu Zantel kwenda Zantel.
Ili kuhahakisha kuwa wateja wa Zantel watanufaika na ofa ya MZUKA, Zantel imezindua pia vacha ya muda wa maongezi ya Tsh 200 ambayo ni ya kwanza Tanzania. Vocha hizi sasa zinapatikana nchini kote.
Bwana Mbaga ameendelea kusema kuwa ili mteja wa Zantel aweze kujiunga na ofa hii atatakiwa kujisajili kwa kupiga *150# au kutuma SMS na neno ‘mzuka’ kwenda namba 150 na hapo hapo wataunganishwa kwenye ya ofa ya MZUKA na kufaidi masaa 12 ya kuongea kwa Tsh 200 tu.
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo Bw. Fintan Lawler ameongeza kuwa kampuni yake inajivunia sana kuzindua ofa hii leo. “Dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma bora bora kwa wateja wetu leo imedhihirika. Masaa 12 ya kuongea kwa Tsh 200 tu ni ofa ya kipekee ambayo tunataraji wateja wetu wataipokea kwa furaha.
‘Mzuka’ ni ofa mpya kabisa ya Zantel ambayo iko juu ya mlolongo wa ofa na huduma za kibunifu zinazolenga katika kutoa huduma bora kwa wateja wake. Huduma nyingine zinazotolewa na Zantel ni pamoja na Sawa Sawa ambapo mteja anatozwa Tsh 3.80 kwa sekunde kupiga simu mtandao wowote hapa nchini masaa 24 nyingine ni 1+ ambapo mteja wa Zantel anapiga simu kwa Tsh 1 kwa sekunde Zantel kwenda Zantel na kujipatia SMS za bure kila wakati anapotumia Tsh 60 kuongea na simu.

0 comments:
Post a Comment