Algeria yaandika historia

Timu ya taifa ya Algeria imeandika historia kwa kupata nafasi bora zaidi katika orodha ya Fifa,kufwatia kufuzu kwake kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Desert Foxes kama wanavyojulikana walihitaji kucheza mechi ya kuamua atakayefuzu kwa kombe hilo dhidi ya wapinzani wao wa Afrika kaskazini Misri ndiyo wapate nafasi ya kwenda Afrika Kusini.
Iko katika nafasi ya 26 kwenye msimamo wa orodha ya dunia na nafasi ya 5 barani Afrika,ikiwa kati ya Misri na Ghana.
Uhispania ndiyo timu bora zaidi duniani ikiwa mbele ya Brazil, ilhali Cameroon ndiyo bora zaidi barani Afrika,ingawa haiko katika orodha ya kumi bora duniani.
Indomitable Lions kama wanavyojulikana wako katika nafasi ya 11,nyuma ya Croatia. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment