RICHARD AKIVINJARI NA KINDA LAKE!!

Richard mshindi wa BigBrother 2007 akiwa na mtoto wake wa kwanza Joshua mwenye umri wa miezi mitano alipokutwa akivinjari na mwanae huyo katika moja ya Hoteli za kitalii leo jijini Dar es salaam, Richard amesema amesimamisha kazi zake ili kumsaidia mke wake katika kumhudumia mtoto wao kwa kuwa mkewe ana majukumu mengi na hawajisikii vyema kumwachia mfanyakazi wakati wana uwezo wa kumlea, nilipoomuuliza Richard kuwa mama yuko wapi alisema "kwa sasa yupo kwenye mkutano hapahapa Hotelini hivyo mimi niko na mtoto na nimechukua majukumu yote ya kumlea".

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment