MISS EAST AFRICA KULAMBA TOYOTA CELICA SPORTS YA DOLA 24.000!!

Mwenyekiti wa kamati ya Miss East Africa na mkurugenzi wa Rena Event Bw. Rena Calist akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach and Resort leo wakati alipotangaza zawadi kwa washindi wa shindano hilo leo linalotarajiwa kufanyika Ijumaa Disemba 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Rena amesema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atazawadiwa gari aina ya Toyota Celica Sports lenye thamani ya dolla 24.000 na pesa taslimu Dolla 3.000 huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja kufanya kazi za kijamii na kampuni hiyo
Mshindi wa pili atajinyakulia kiasi cha dolla 2.000 na mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya Rena Event pia na mshindi wa tatu atajinyakulia dolla za marekani 1.000, shindano hilo linashirikisha warembo 14 wawili kutoka kila nchi 7 zilizotuma wawakilishi wa nchi zao, nchi hizo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania Somalia na Mouritius.
Burudani zitaporomoshwa na mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Ferre Gola kwa kushirikiana na wanamuziki wengine wa hapa nyumbani, anayeonekana kushoto katika picha ni Judith Kimeshi meneja masoko wa Kunduchi Beach Hotel and Resort
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Miss East Afrika linalotarajiwa kufanyika disema 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City wakiwa wamepozi pembeni mwa gari la zawadi ya mshindi wa shindano hilo aina ya Toyota Celica Sports kwenye hoteli ya Kunduchi beach and Resort leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment