Kim akizungumza na waandishi wa habari katika moja ya mikutano aliyowahi kufanya na wanahabari kwa ajili ya burudani.
Habari zilizotufikia Hivi Punde zinasema DJ wa siku nyingi AbdulhaKhim Magomelo (Dj. Kim and The Boy) amefariki dunia katika Hospitali ya Saint Monica iliyoko Manzese jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa
Habari kutoka kwa shemeji wa Marehemu Bw. Mohamed Bawazir zinasema Kim Amefariki saa kumi jioni leo na alikuwa amelazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid), Kim atakumbukwa na watu mbalimbali waliokuwa wakifuatilia muziki wa Disco enzi hizo na hasa mashindano mbali mbali ya madansa kwani ndiyo mwandaaji wa kwanza wa mashindano hayo hapa nchini na alikuwa akitoa mchango mkubwa katika masuala mazima ya burudani
Tutawaletea habari zaidi na taarifa za msiba huo kadiri tutakavyozipata
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.
2 comments:
Mwenye ezi Mungu amuweke Mahala Pema Peponi, Amina.
Mwenye ezi Mungu amuweke Mahala Pema Peponi, Amina.
Dah, nimepatwa na simanzi kubwa! Kaka katangulia, siamini! Ghafla kumbukumbu ya mambo mengi inanirudia! Miaka kibao ya matamasha na ubunifu! Kim alikuwa mtu mwema sana! Mcheshi, mwenye heshima na "fighter" halisi.
Weasiwasi wangu ni kwamba kinara huyu wa ukuzaji burudani ametutoka na huku nyuma hatuna namna ya kumuenzi.
Wasanii wote wa Kikzazi kipya wanatakiwa wamtambue Kim!
TUSIMSAHAU TAFADHALI!
Dah, nguzo ya Historia ya Burudani Tanzania hiyo imeanguka!
Taji
Post a Comment