Waziri Kamara mgeni rasmi Miss East Africa!

Dk. Deodarus Kamara
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Deodarus Kamara atakuwa mgeni rasmi katika shindano la Miss East Africa litakalofanyika ijumaa hii kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Miss East Africa, Petter Mwendapole alisema wamemwalika Waziri huyo kwa kuwa mashindano hayo yako kwenye ukanda wake.“Waziri Kamara ndiye mwenye Afrika Mashariki na mashindano haya yanahusisha eneo hili sasa ni vyema akawa mwenyewe akazungumzia habari ya ukanda wetu,” alisema.Mwendapole alisema tayari Waziri Kamara amethibitisha kuwepo kwenye shindano hilo ambalo pia linatarajia kushuhudiwa na mawaziri wengine wa nchi za Afrika Mashariki.Miss East Africa inafanyika Mlimani City ambapo nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Tanzania, Mauritius, Djobouti na Somalia.Tiketi za shindano hilo zinauzwa kwa sh 100,000 ambapo watakaolipa watapewa na chakula, tiketi za kawaida zitakuwa sh 50,000 ambapo zinauzwa Movenpick Hotel, Steers, Tina Maria Boutique, Samaki Samaki Mlimani City, Kunduchi Beach Hoteli, TCC Club Chang’ombe, Engen Mwenge, Engen Ubungo, Sea Cliff, Msasani Sleepway.Miss East Africa inaandaliwa na Rena Event na kudhaminiwa na CMC, Kunduchi Beach Hotel, New Habari (2006) Limited, DD Whole Sale, East Africa Radio na Televisheni, Ako Catering Service.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment