Mpiga solo maarufu wa Bendi ya African Stars, Shakashia akionyesha umahiri wake katika kupiga gitaa wakati wa onyesho lao lililofanyika usiku wakuamkia leo na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki kwenye ukumbi wa Mango Garden-Kinondoni jijini Dar es Salaam huku waimbaji wa bendi hiyo Furgason (kushoto) akifuatiwa na Kalala Junior na Salehe Kupaza (kulia) wakisikilizia mirindimo.
Bendi hiyo imeendelea kujizatiti zaidi katika kuimarisha ubora wa Muziki wake mara baada yakutoa album yao mpya ya 'MWANA DAR ES SALAAM' iliyozinduliwa mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee, na katika onyesho lao la jana ambalo mwakilishi wa FULL SHANGWE alihudhuria, kulikuwepo na utulivu wa hali ya juu katika kila chombo kilichopigwa, ikimaanisha burudani yote kwa ujumla ilisikika kwa ufasaha jambo ambalo liliwafanya mashabiki wapige swaga lakufa mtu!
Furgason na Diof wakirap' usiku wa kuamkia leo walipokuwa wakitoa burudani kwa mashabiki wa African Stars.
Mwimbaji mahiri wa kike katika bendi hiyo, Luiza Mbutu hakuwa nyuma kuonyesha uwezo wake sambamba na wanenguaji wengine!
0 comments:
Post a Comment