TIMU ya soka ya African Lyon, imemchukua nahodha wa zamani wa klabu ya Simba, Seleman Matola, kuwa kocha wake msaidizi.Matola aliyekuwa pia kocha wa timu ya vijana ya Simba, chini ya miaka (20), atakuwa chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu hiyo, Kambi Mbwana, alisema kwamba kumchukua kocha huyo, kutaiweka klabu yao katika mazingira mazuri.Alisema uzoefu mkubwa wa Matola katika maisha yake ya soka, ni jambo liliowafanya washawishike kuwa naye ndani ya timu yao.“Tupo kwenye kipindi cha kujiweka sawa kabla ya Ligi kuanza Januari mwakani, hivyo uongozi umeona umchukuwe Matola kuwa kocha msaidizi,” alisema.“Naamini akishirikiana sambamba na kocha wetu, Boniface Mkwasa, mambo yatakuwa mazuri zaidi.”African Lyon inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini na mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewji ‘Mo’, ilipanda daraja mapema mwaka huu sambamba na Majimaji na Manyema Rangers.
SULEIMAN MATOLA KOCHA MSAIDIZI WA AFRICA LYON!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment