DOWUTA WATILIANA SAINI NA TICTIS JUU YA UBORESHAJI WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI!!

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Bandari Tanzania (DOWUTA) Bw. Abdalla Kibunda (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS), Bw. Neville Bissett mara tu baada ya kutiliana saini mkataba wa ‘Hali Bora kwa Wafanyakazi’ kwenye bandari ya Dar leo. Mkataba huo una lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwenye bandari ya Dar es salaam (Picha: Hisani ya Executive Solutions)
MSC MAGALI, meli kubwa zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari ya Dar es salaam leo iliwasili katika gati la Kampuni ya Kuhudumia Makontena Bandarini (TICTS). Meli hiyo iliyotokea Salalah nchini Oman ina urefu wa mita 234 na upana wa mita 32 (Picha: Hisani ya Executive Solutions)



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment