Mwenyekiti wa kamati ya Miss East Africa na mkurugenzi wa Rena Event Rena Calist kulia akisalimiana na Rais mstaafu wa Burundi Pierrre Buyoya wakati wa shindano hilo lililofanyika nchini humo mwaka jana.
ZAWADI za washindi wa shindano la Miss East Africa zinatarajiwa kutangazwa leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss East Africa, Rena Callist Amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba watataja zawadi hizo katika mkutano wao na waandishi wa habari.“Kesho tutangaza zawadi kwa ajili ya washindi wa shindano la Miss East Africa ambalo fainali zake ni Ijumaa pale Mlimani City, zawadi hizi zitakuwa nzuri na nono kwa washindi wote,” alisema.Alipoulizwa kama mshindi wa mwaka huu atapewa gari kama alivyopewa mshindi wa mwaka jana, Rena alisema baada ya mkutano kila kitu kitakuwa wazi.“Mwaka jana tulitoa gari Lexus ambalo lilikwenda Burundi lakini tunaahidi zawadi ya mwaka huu kwa mshindi wa kwanza na wale wanaomfatia itakuwa nzuri,” alisema.Claudia Niyonzima alishinda taji hilo na kuzawadiwa gari hilo lenye thamani ya zaidi sh milioni 40.
Shindano hilo linadhaminiwa na gazeti la The African linalochapishwa na New Habari (2006) Limited, Kunduchi Beach Hotel, Ako Catering, Events Lights, Valley Spring, DD Whole Sale, CMC Auto Mobile.
0 comments:
Post a Comment