SIMBA NA SOFAPAKA ZATOKA SULUHU KOMBE LA TUSKER!!

Kikosi cha timu ya Simba ya Tanzania.
Kikosi cha timu ya Sofapaka ya Kenya.

Timu ya Simba ya Tanzania na Sofapaka ya Kenya zimetoka suluhu katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo, mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza kwa simba toka mashindano ya kombe la Tusker yaanze wiki hii wakati Mtibwa Sugar na Sofapaka zilipofungua dimba la michezo hiyo ambayo timu ya Sofapaka iliishinda Mtibwa Sugar 3-1.
Timu hizo katika mchezo wao wa leo zimeonyesha kiwango kizuri kinachofanana hivyo kuzifanya zitoshane nguvu kwa kutoka uwanjani bila kufungana, hata hivyo Simba itabidi wajutie nafasi waliyoipata baada ya mchezaji wake Mussa Hassan Mgosi kukosa Penati katika kipindi cha kwanza Cha mchezo huo.
Mpaka mchezo huo unamalizika katika uwanja wa Uhuru hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie na hivyo kuzifanya timu hizo kugawana pointi 1 kila timu, kwa matokeao hayo Sofapaka ya Kenya imefikisha pointi 4 baada ya kushinda mchezo wa kwanza na imetinga nusu fainali huku Simba na Mtibwa zikisubiri mchezo wao ili kujua nani atakwenda nusu fainali, katika mchezo huo mshindi yoyote kati ya Mtibwa Sugar na Simba anaweza kucheza nusu fainali

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment