Senegal yapata kocha mpya

Shirikisho la Soka nchini Senegal (FSF) limemteua Amara Traore kuwa kocha mpya wa timu yao ya taifa inayojulikana kama Teranga Lions.
Traore mwenye umri wa miaka 44 na mchezaji wa zamani amefunza timu ya daraja la kwanza ya ASC Linguere de St-Louis tangu mwaka 2007, na kuwasaidia kuchukua ubingwa msimu huu.
Senegal imekuwa bila kocha tangu Oktoba 2008 baada ya Lamine Ndiaye kufutwa kazi kwa kushindwa kuiwezesha timu kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Jukumu lake la kwanza ni kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa barani Afrika 2012 na michezo ya Olimpiki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment