Katika sikukuu ya Krismass na mwaka mpya kampuni ya simu ya Zain imeandaa kikundi cha sarakasi cha Sarakasi Mama Afrika kitakachokuwa kikitoa burudani jijini Arusha katika viwanja vya AICC kijenge mjini Arusha kuanzia Disemba 15 2009 kwa kipindi cha wiki nne.
hii itakuwa ni mara ya pili kwa kikundi hicho cha Sarakasi Mama Afrika kufanya shoo mkoani humo baada ya mafanikio makubwa ya kundi hilo wakati lilipofanya onyesha kama hilo mkoani humo mwaka jana.
Tiketi zitauzwa kwa shilingi 8.000 kwa viti vya kawaida na elfu 12.000 kwa viti maalum yaani VIP.
0 comments:
Post a Comment