Meneja wa tawi la Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Tawi la KinondoniHaigath Kitala kulia akimkabidhi hundi ya shilingi 300.000 mwenyekiti wa Buibui Queen Zuwena rajabu na mteja wa PTF tawi la Kinondoni sentaya Kambangwa B kwa ajili ya kuwasaidia kwenye mashindano yanayoendelea mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni Meshack Kussaja afisa wa tawi hilo naHilda Kayombo mteja wa Taasisi hiyo, makabidhiano hayo yamefanyika leokwenye tawi hilo lililopo Mwenge Afrika Sana.
Taasisi hiyo ya kifedha inatoa mikopo kwa makundi mbalimbali kama vile wajasiliamali, wafanyakazi wa kima cha chini, Jeshi la Polisi, Mikopo ya Nyumba na Ada za shule kwa watoto na mikopo ya uwezeshaji kama vile SACCOS na mikopo hii ni kuanzia shilingi 100.000 mpaka milioni 20.000.000
0 comments:
Post a Comment