Grace Kilembe Meneja Mradi wa Kisura akizungumza na wanahabari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo kulia ni Emmy Melau Kisura wa Tanzania 2008.
Baadhi ya washiriki wa kisura wa Tanzania 2009 wakiwa katika picha ya pamoja.
Kampuni ya Beautful Tanzanie Agency imetangaza zawadi za washindi wa shindano hilo la kisura wa Tanzania 2009 na kusema kuwa mshindi ataibuka na kitita cha shilingi 5,000.000 na kupata mkataba wa kufaya kazi za Serengeti Breweriers kwa mkataba wa mwaka mzima kama balozi wa kampuni hiyo.
Shindano hilo lianatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Movenpick disemba 17 kuanzia saa 1.00 usiku ambapo jumla ya washiriki 10 wamefanikiwa kutinga Fainali ya shindano hilo ambalo mwaka huu linafanyika kwa mara ya pili mfurulizo.
Utaratiobu uliotumika kuwachuja washiriki hawa ulikuwa ni kwa njia ya kupiga kura watanzania na watazamaji walipiga kura kupitia televisheni ya taifa TBC1 kwa kutuma SMS kwenda namba 15771 kwa wiki mara tatu jumapili, jumanne, na ijumaa.
Kwa sasa washiriki bado wapo kambini kwenye Hoteli ya Kiromo View Resort iliyoko Bagamoyo Pwani chini ya Mkufunzi wao Emmy Melau ambaye ni kisura wa Tanzania mwaka 2008 kutoka mkoani Arusha.
0 comments:
Post a Comment