Mwanadiplomasia atimuliwa Tanzania!!


Mwanadiplomasia mmoja kutoka Canada aliyemtemea mate polisi na mwandishi wa habari nchini Tanzania anarejeshwa kwao.
Balozi wa Canada Robert Orr aliitwa na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kuzungumiza tukio hilo wiki iliyopita.
Bw Orr alisema, "Kwa faida ya nchi zote mbili, afisa huyo wa Canada ataondoka nchini Tanzania haraka iwezekanavyo."
Hata hivyo, mwandishi wa habari aliyetemewa mate na mwanadiplomasia huyo amesema bado anataka kuchukua hatua za kisheria.
Jerry Muro anayeonekana akiwa ameshikilia cheti katika picha na anayefanya shirika la habari la taifa TBC ameliambia gazeti moja la HabariLeo nchini humo , "Haki lazima itendeke. Kumrejesha ni hatua moja tu, lakini haimaanishi kwamba yamekwisha. Nitakwenda polisi kuhakikisha wanashikilia hati yake ya kusafria." na http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment