Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Zain Tanzania, Muganyizi Mutta akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha la wanahabari wa vyombo tofauti litakalofanyika kwenye viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama Desemba 19, mwaka huu chini ya udhamini wa Zain na uratibu wa Kampuni ya Capital Plus International (CPI). Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe. (Picha na Rajabu Mhamila)
KAMPUNI ya simu za mkononi Zain, imeandaa Tamasha la waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari litakalofanyika Desemba 19 mwaka huu katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Muganyizi Mutta, alisema hatua hiyo ni katika kutambua mchango wa vyombo vya habari kwa jamii katika kuhabarisha, kushawishi na hata kuburudisha.
Alisema wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kwamba Zain wameona ni kitendo cha uungwana kwao kuonyesha thamani waliyonayo wanahabari kwa kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo.
“Ni kawaida katika kila mwisho wa mwaka kufanya tathimini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda lakini pia huwa tunakitumia kipindi kukaa na kufurahi kwa pamoja na watu wenye majukumu tofauti katika kulijenga taifa ambapo miongoni mwao ni nyinyi wanahabari,” alisema Mutta.
Mutta alisema pamoja na burudani tofauti pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya kubahatisha ambapo wanahabari wataweza kujishindia zawadi tofauti kutoka Zain.
Tamasha hilo limeratibiwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambapo Mratibu wake Mawazo Waziri aliitaja michezo itakayochezwa kuwa ni mpira wa miguu, netiboli na kuvuta kamba ambapo katika burudani kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza muziki wa dansi.

0 comments:
Post a Comment