MWANAMUZIKI Ferre Batangire Gola ‘Shetani’ kutoka Jamhuri ya Kidemokarsi ya Kongo anatarajiwa kutua nchini kesho kwa ajili ya kutumbuiza kwenye onyesho la Miss Eas Africa.Mbali na Ferre mwanamuziki mwingine maarufu Afrika Mashariki Kidumu Kinene wa Kenya ambaye ni raia wa Burundi atatumbuiza pia kwenye shindano hilo.Mwenyekiti wa Miss East Africa, Rena Callist alisema jana mjini Dar es Salaam kwamba wanamuziki hao wamethibitisha kuwepo kwenye onyesho hilo.“Tayari tumekwishamalizana nao na Ferre atawasili hapa kesho kwa ajili ya onyesho la Ijumaa na atafanya mkutano na waandishi wa habari,” alisema.Kuhusu wasanii wa ndani, Rena alisema msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Vumilia Mwaipopo ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake za Utanikumbuka, Tatizo Umaskini atakuwepo kunogesha shoo hiyo.“Kidumu hii ni mara yake ya kwanza kutumbuiza Tanzania, kama ilivyo kwa Ferre lakini pia tumempa nafasi Vumi akiwa na bendi yake ya K-Mondo Sound watakuwepo kuhakikisha kwamba Tanzania inawakilishwa.”Alisema pia kuwa kutakuwa na kikundi cha ngoma za asili. K-Mondo ina nyota wengine pia kama Richard Mangustino na Mhina Panduka ‘Toto Tundu’.Miss East Africa inafanyika hii kwenye ukumbi wa Mlimani City ambapo kiingilio kitakuwa sh 100,000 kwa viti maalum ambapo watakaolipa watapewa na chakula, sh 50,000 kwa viti vya kawaida.Shindano hilo linadhaminiwa na gazeti la The African linalochapishwa na New Habari (2006) Limited, Kunduchi Beach Hotel, Ako Catering, Events Lights, Valley Spring, DD Whole Sale, CMC Auto Mobile.
FERRE GOLA KUTUMBUIZA MISS EAST AFRICA IJUMAA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment