WENGI WAFURAHIA HUDUMA ZA MTANDAO WA SASATEL!!

Safina Mchomvu mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Sasatel Tawi la Libya akimuelezea mteja bwana Tedla Belayneh jinsi ya kutumia mtandao wa Intanet wa kampuni hiyo, wakati mteja huyo alipokwenda dukani hapo kujipatia huduma za intanet, Sasatel imekuwa ikijiimarisha zaidi kwa kupanua huduma zake za mawasiliano kwa njia ya simu za mkononi, mezani na mtandao wa Intanet.
Thomas Mgondah msimamizi wa Duka la Kampuni ya simu za mkononi Sasatel tawi la Libya na Jamhuri akielekeza jambo kwa mmoja wa wafanyakazi wa duka hilo Caren Kahema aliyesimama nyuma huku mfanyakazi mwingine Saiphon Asajile akiongea na wateja kwa njia ya simu tayari kwa kuwapelekea huduma ya mtandao huo pale walipo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment