Baada ya kasheshe Woods apumzika Golf!

Mcheza Gofu Tiger Woods.

Tiger Woods ameamua kupumzika kwa muda usiojulika kucheza gofu ili aweze kukabiliana na matatizo yanayoizonga familia yake hivi sasa.
Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wake amesema anafahamu namna alivyowakasirisha wapenzi wa mchezo wa gofu kutokana na kukosa uaminifu alikoisababishia familia yake.
Mcheza gofu huyo anayeshikilia nafasi ya kwanza duniani anajaribu kutengeza pale alipoharibu na ameomba faragha kwa familia yake.
Wadhamini wakubwa wa Woods kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imesema itaendelea kufanya kazi nae, lakini wakala wake amesema ni mapema mno kuzungumzia athari za kibiashara anazofanya.
Kupitia mtandao wake Woods ameomba msamaha na kutaka asamehewe.
Habari na www.bbcswahili.com .

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment