Meneja mkuu wa Makampuni ya Shivacom Parthiban C. wa pili kutoka kulia na Meneja wa udhamini na mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za Gari aina ya Suzuki Grand Vitara Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald katika duka la kampuni hiyo lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam, Gari hilo jipya lina thamani ya shilingi milioni 53 na litamsaidia mrembo huyo katika kazi zake mbalimbali za kijamii Miriam Gerald alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar es salaam na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
VODACOM MISS TANZANIA AKABIDHIWA MCHUMA WAKE LEO!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Mimi Cjui Tanzania inakwenda wapi?Miss Tanzania ni Wa Mwanza atakabidhiwaje Dar au ndo Mapendesheee watoa Zawadi wanataka hela zao zirudi lipelekeni Mwanza.
Post a Comment