Prof. Jumanne Magembe Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Na Anna Nkinda - Maelezo, Chunya
03/11/2009 Serikali imeombwa kujenga mabweni angalau mawili katika kila shule wilayani Chunya kwa ajili ya wanafunzi wasichana wanaotoka katika jamii ya wafugaji, wavuvi na wachimbaji ambao wazazi wao wana tabia ya kuhamahama na kusababisha adha kwa wanafunzi hao.
Ombi hilo limetolewa jana na wanafunzi wa kike wa wilaya hiyo wakati wakisoma risala yao kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo na hivyo kupata muda wa kuongea na wanafunzi hao katika ukumbi wa Moon Light.
Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wenzake Pendo Gabriel ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kiwanja alisema kuwa hivi sasa wanafunzi wengi wanaotoka katika jamii hiyo wamekuwa wakipanga mitaani na hivyo kupata kero mbalimbali ambazo zinawapotezea muda wa kujisomea.
"Tunaamini kuwa kujengwa kwa mabweni hao kutaondoa adha ya kupanga nyumba mitaani na kupunguza vishawishi vibaya ambavyo vingeweza kusababisha kupatikana kwa mimba zisizotarajiwa kwani ndani ya miaka minne tangu mwaka 206 hadi mwaka huu wanafunzi wenzetu 114 wa shule za sekondari wamepata ujauzito na hivyo kukatiza masomoyao", alisema Pendo.
Aidha wanafunzi hao pia waliiomba Wizara ya Nishati na Madini kupitia shirika lake la Umeme Nchini (TANESCO) kuweka kipaumbele katika kuzipatia umeme shule za sekondari zilizo karibu na gridi ya Taifa kwa gharama nafuu.
Akiongea na wanafunzi hao Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa hivi sasa Serikali inalipa kipaombele suala la elimu hapa nchini kwa kuhakikisha kuwa kila kata inakuwa na Shule ya Sekondari.
"Mnachotakiwa kufanya ninyi kama wanafunzi ni kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi ambavyo vitawasababishia kupata Ugonjwa wa UKIMWI na mimba za utotoni na hivyo kukatisha masomo yenu", alisema Mama Kikwete.
Taasisi ya WAMA iliwapatia wanafunzi hao zawadi za jezi pamoja na mipira ambayo wataitumia katika mazoezi mara baada ya kumaliza muda wa masomo yao.
Wilaya ya Chunya ina shule za Sekondari 20 kati ya hizo 18 ni za Serikali na mbili zinamilikiwa na Jumuia ya wazazi na idadi ya wanafunzi katika shule za Serikali ni 5690 wasichana ni 2,404 na wavulana 3286.

0 comments:
Post a Comment