Kivumbi cha kumpata mrembo wa Fainali za Miss Utalii Ilala 2009 ni tarehe 6/11/2009 Ijumaa katika ukumbi wa Da’ West Park Inn Tabata, ambapo jumla ya Warembo 12 watapanda katika jukwaa kuchuana kuwania taji kwa musimu wa 2009/2010.Katika shindano hilo ambalo macho na masikio kwa wakazi wa Dar es Salaam limewatia wazimu kutokana na kutoelewa nani hataibua nderemo, Vifijo, na makelele kutokana na warembo wote kuwa katika hali ya Ushindani mkali ambapo kila mrembo amejigamba kuibuka na taji hilo kasha kubeba vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha thamani yake ikiwa ni milioni mbili .Warembo hao walioanza kambi kwa takribani mwezi mmoja katika Ukumbi wa Da’ West Park Inn-Tabata, waliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii unaopatikana Tanzania ikiwemo Hifadhi za Utalii za Taifa, Vivutio vya Kitalii, pamoja na Maajabu ya Dunia yanayopatikana hapa Tanzania.Aidha katika shindano hilo, warembo hao wataonyesha Mavazi ya asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania, watacheza ngoma kuonyesha utamaduni wa Mtanzania, Watavaa mavazi ya Kitanzania ya Kitalii, vazi la Ubunifu lililotengenezwa kwa maligafi za hapa Tanzania, pamoja na mengine mengi yanayohusiana na masuala ya Utamaduni wa Mtanzania.
Miss Utalii Ilala katika Msimu huu ilipata bahati ya Kuungwa Mkono kwa asilimia mia moja na Mkurugenzi wa Chicken Hut Tanzania ltd ya Mlimani City, Savannah Lounge- Paradise City Hotel iliyopo katika jingo la Benjamini Mkapa Tower-Posta Mpya, Chaga Bite iliyopo Kijitonyama, Kampala International University iliyopo Gongolamboto, pamoja na Ukumbi wa Da’ West Park Inn- Tabata.Wadhamini wengine waliojitokeza kuunga mkono ni wadau wa Shindano la Miss Utalii ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
0 comments:
Post a Comment