Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) (kulia) akimkabidhi picha ya nembo ya WAMA Mkurugenzi wa Mipango wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Tanzania Robert Cunnane (kushoto) wakati alipozitembelea ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam
Na Anna Nkinda – Maelezo
Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Tanzania limeahidi kushirikiana na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) katika kutekeleza miradi ya kupunguza mimba za utotoni ili kumwezesha mtoto wa kitanzania kusoma na kuwa na maisha mazuri hapo baadaye.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa Mipango wa USAID Robert Cunnane alipokuwa akiongea na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipozitembelea ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona jinsi gani wanaweza kuisaidia Taasisi hiyo ambayo moja ya shughuli zake kubwa ni kushughulikia mambo ya afya na elimu.
Cunnane alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi na WAMA katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupambana na ugonjwa wa UKIMWI na hivi sasa wameamua kumuendeleza mtoto wa kike kwa kupunguza mimba za utotoni kwa maendeleo ya watanzania.
Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA alilishukuru Shirika hilo kwa kumsaidia mtoto wa kike na kuwaomba waongeze fursa zaidi hasa katika rasilimali fedha kwa kujenga mambweni ya wasichana ili watoto wakae karibu na shule jambo ambalo litasaidia kupunguza mimba mashuleni.
“Shirika hili limekuwa likifanya shughuli mbalimbali za kumuendeleza mtoto wa kike kwani katika shule ya Sekondari ya Ngongo iliyopo mkoani Lindi wamejenga mabweni mawili ya wanafunzi wa kike ambapo jumla la watoto 45 wanaishi katika mabweni hayo”, alisema Mama Kikwete.
Katika kutekeleza miradi hiyo USAID watatoa fedha na msaada wa kiufundi ambapo Taasisi ya WAWA watatoa mwongozo wa urakibishi.

0 comments:
Post a Comment