Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kushoto akimkabidhi katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na waamuzi watakaochezesha ligi Ligi kuu ya Vodacom, makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye Hoteli ya Girrafe iliyoko mbezi Beach, msimu huu wa 2009-2010 Vodacom itatumia jumla ya shilingi bilioni 1.1 kwa uendeshaji wa ligi hiyo ya Vodacaom ikiwa ni udhamini wa uendeshaji wa mashindano hayo.
Naibu Waziri Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kulia akimkabidhi Jezi katibu mkuu wa Timu ya Simba Mwina Kaduguda aka (Simba wa Yuda) Timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimekabidhiwa vifaa vitakavyotumiwa na na timu katika michezo yao leo katika hoteli ya Girrafe iliyoko Mbezi Beach jijini Dar katikati wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa masoko Vodacom Ephraim Mafuri na Mkuu wa kitengo cha Udhamini na Mawasiliano George Rwehumbiza.
Naibu Waziri wa Habari Michezo na Utamaduni Joel Bendera kulia akimkabidhi Jezi na mpira Katibu mkuu wa timu ya Yanga Lucas Kisasa huku, Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Ephraim Mafuru akiangalia, Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom zimekabidhiwa vifaa vitakavyotumika kwenye michezo yote ya ligi hiyo, hafla hiyo imefanyika kwenye Hoteli ya Girrafe iliyoko Mbezi jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment