Murugenzi wa kampuni ya simu za mkononi Sasatel Christian Haeger kulia akizungumza na Mkuu wa Idara ya fedha wa kampuni hiyo bw.Andre Lort mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliokutanisha wakurugenzi wa makampuni mabilmbali jijini na kampuni hiyo ili kuwaelezea jinsi kampuni hiyo inayotoa huduma, ubora wa bidhaa zake na jinsi zinayofanya kazi ya mawasiliano, kampuni ya Sasatel inatoa huduma ya simu za mkononi, mezani na kuwaunganisha wateja wake na mtandao yaani Internet
Meneja Masoko na Mauzo wa Sasatel Derick Byarugaba kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Gerrad Massane Meneja huduma na mauzo ya Rejareja Retail Manager mara baada ya mkutano huo.
kutoka kulia ni Frank Semaganga Afisa Bidhaa wa Sasatel akiwaelekeza kitu wafanyakazi wenzie wa kampuni hiyo Mayjodal Essaji katikati na John Warrange mkuu wa mauzo kulia.
Mkuu wa Idara ya Fedha Sasatel Andy Rolt kulia akizungumza na mmoja wa wageni mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa Sasatel uliohudhuriwa na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali jijini na kupata mambo mbalimbali yanayohusu huduma ya kampuni ya simu ya Sasatel na bidhaa zake.
Renny Nindi ambaye ni key accountant Manager akimwelezea mmoja wa wageni katika mkutano huo jinsi simu za kampuni hiyo zinavyofanya kazi leo kwenye hoteli ya Movenpick wengine katika picha ni Erick M. Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka PME London Uingereza na mmoja wa washia dau wa Sasatel na katikati ni Frank Semaganga Afisa Bidhaa wa Sasatel.
0 comments:
Post a Comment