Hatimae Miriam Gerald mrembo kutoka mkoa mwanza amenyakua taji la Vodacom Miss lake Zone,kulia kwake ni mrembo Mary Charles Alieshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikirudi hukohuko mara kwa mrembo Sabina Budodi,namba nne ikishikiliwa na Glory Inosent mrembo kutoka Shinyanga,na namba tano alichukua mrembo Emakulata Alphonce kutoka Kagera,
Mgeni rasmi katika shindano hilo alikuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa ushirikiano Afrika mashariki,Mohamed Aboud ambaye aliwakabidhi washindi zawadi zao hapohapo namba moja alipewa fedha taslim 600.000 huku aliechukua nafasi ya pili akiondoka na kitita cha 400.000, na mshindi wa tatu shilingi 300.000, mshindi wa nne na wa tano walipewa shilingi 150.000 kila mmoja na warembo wote walipewa zawadi zao isipokuwa mrembo namba tano Emakulata Alphonce kutoka kagera ambaye alipatwa na mshtuko na kupoteza fahamu alipotajwa na jaji mkuu kwamba ameshika namba tano,hivyo hakuweza kufika mbele kwani alikuwa amepelekwa hospitali ya rufaa bugando,tunamshukuru mungu kwani kwa sasa anaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment