MISS EAST AFRICA YAZINDUA BAHATI NASIBU YA RANGE VOGUE SPORT!!

Mkurugenzi wa Lena Event inayoandaa Miss East Africa Lena Calist akionyesha gari aina ya Range Vogue Sport lenye thamani ya dola za Kimarekani 165.000 litakaloshindaniwa katika bahati nasibu ya Miss East Africa iatakayoanza kesho mpaka siku ya fainali ya Miss East Africa itakayofanyika desema 18 2009 jijini Dar es salaam, Lena ameongeza kwamba ili kucheza bahati nasibu hiyo utatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 1000 au kucheza kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote ukituma neno SHINDA kwenda namba 15567 kwa shilingi 1000 na kujipatia nafasi zaidi ya kushinda zawadi hiyo ya Gari, Fedha zitakazopatikana katika bahati nasibu hiyo zitapelekwa katika vituo vya watoto yatima wa Burundi na kituo cha watoto yatima cha Saint Teresa Children Cha jijini
Shindano hilo mwaka huu litashirikisha nchi 14 na kila nchi itawakilishwa na warembo 2, wengine waliopo katika picha ni Foti Gwebe Nyirenda Mshauri wa Mauzo CMC Motors na katikati ni Miss East Africa namba mbili mwaka 2008 Annete John.
Mkurugenzi wa Lena Event Lena Calist akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski leo wakati wa uzinduzi rasmi wa bahati nasibu ya Miss East Africa ambapo gari aina ya Range Vogue Sports litashindaniwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment