WALIOENDA KWA BAISKELI TANGA WAREJEA TENA DAR!!

Waendesha Baiskeli kutoka chama cha Baiskeli Mkoa wa Dar es salaam kutoka kushoto Said kengele katibu wa (CHABADA), Kiboi Mbwana, Moshi Mfinanga na Mussa Haussein, ambao waliondoka hivi karibuni kwenda Mkoani Tanga kwa kutumia Baiskeli zao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kurejea jijini leo asubuhi wakitokea mkoani humo, ambapo lengo la mbio hizi za waendesha Baiskeli ilikuwa ni kuhamasisha jamii ya kitanzania kutembelea vivutio vya utalii vya ndani na kuhamasisha watu kutumia baiskeli kama usafiri na kuendeleza mchezo wa kuendesha baiskeli.
Kengele amesema wamekubaliana kuwa na urafiki na chama cha Baiskeli mkoa wa Tanga (CHABATA)ambapo watakuwa na utaratibu wa kutembeleana na kuandaa mashindano ya mbio za Baiskeli kwa pamoja, wengine waliofanikiwa kumaliza mbio hizo ni waendesha baiskeli Alen Nyanginywa,Bashir Bakari .na Ally Bakari.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment