WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA- AWAASA WANANCHI KUTUMIA M- PESA!!

Mbunge wa viti maaalum, Al-Shymaa Kwegyir, akipita jukwaani na vazi la ubunifu, wakati wa onyesho hilo, lililofanyika kwenye Ukumbi wa bunge mjini Dodoma juzi.
Wabunge walioshiriki onyesho la mavazi, lililoandaliwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom na wabunifu wa mitindo maarufu wa nchini, wakiwa jukwaani na mbunifu aliyebuni mavazi waliyovaa kwenye onyesho hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa bunge mjini Dodoma.

Mh.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongelea jambo wakati wa hafla ya meet and greet iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania na kutoa somo kuhusu huduma ya M-Pesa.(kulia)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare.

Na mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewaasa wananchi na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia huduma ya M-pesa inayotolewa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania na kuwataka wabunge na Watanzania kuitumia huduma hiyo kwa kutuma na kuchukua fedha ili kuokoa muda wanaoupoteza wanapokwenda kupata huduma hiyo sehemu nyingine na kuwaomba wabunge kuwaelimisha wananchi majimboni mwao.
Pinda alitoa wito huo jana usiku alipokuwa kwenye hafla ya meet and greet ambapo kampuni ya simu ya vodacom ilichukua furusa hiyo kwa ajili ya kuelezea huduma za M-pesa pamoja na zoezi la usajili wa laini za simu (Simcard)
Waziri mkuu alisema M-pesa ni huduma bora kwa kuwa humfanya mtu kutokwenda kupanga foleni ya kutuma, kupokea au kuchukua fedha katika taasisi zinazojihusiha na fedha pia ni huduma inayoweza kumsaidia mtanzania kununua Luku,kulipa bili ya maji Dawasco na kupokea mishahara yao kupitia njia hii kiurahisi zaidi.
“hawa jamaa (Vodacom) walipokuja kunieleza huduma hii, niliwaambia ni vema habari hii wakaifikisha kwa wabunge kwa kuwa wao wanaweza kuifikisha vizuri zaidi kwa wananchi” alisema Pinda
Pinda alisemaa kutokanaa na kuhamishaa huko haata yeye atanza kuitumia huduma ya M-pesa pamoja na kusajili laini ya simu yake ili aweze kwenda na mabadiliko ya teknolojia.
“kesho na mimi nitakwenda kusajili simu yangu, nimeelezwa hapa bungeni kuna vibanda vinatoa hudumaa hiyo” alisema Pinda.
Naye meneja wa Vodacom Innocent Ephraim, ambae ni mtaalamu wa huduma ya M-pesa alisema ni huduma nzuri kwa kuwa haimfanyi mtu kutembea na fedha nyingi lakini pia hurahisisha zoezi la kutuma na kupokea fedha.
Alisema zoezi hilo lina manufaa zaidi kwa kuwa hata maeneo ya vijijini yasiyo na taasisi za kifedha huweza kunufaika na mfumo huo uliobuniwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya mtumiaji wa mtandao huo.
Aidha kuhusu zoezi la usajili wa simu, alisema mawakala mbalimbali wa mkoani hapa wanatoa huduma hiyo ili mradi mtu awe na vitambulisho vinaavyotakiwa.
“zoezi la usajili wa laini si lazima uende Dar es salaam au sehemu nyinginezo kwa kuwa hata mawakala wa hapa wanatoa huduma hiyo” alisema mtaalamu huyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Mzengwa kidole na jicho please.

Post a Comment