Bonanza la Bunge Stars na TBL lafana mjini Dodoma!!

Mchezaji Omari Ali wa Bunge Stars (kushoto) akipambana na Fadhili Ali wa timu ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na TBL, juzi kwenye viwanja vya Jamhuri, Dodoma. TBL ilishinda mabao 3-1.
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Lucy Kiwelu (kulia) wa timu ya Bunge queens akijiandaa kufunga huku akikabwa na Tabia Mhusi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika pambano la netiboli lililofanyika wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na TBL, juzi uwanja wa Jamhuri, Dodoma.Kushoto ni Dafloza Atilio wa Bunge Queens. Bunge Queens ilishinda 14-7.

Mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Tunu Pinda (wa pili kushoto) akijumuiaka kucheza muziki pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Konyagi, Kiroi Suma (kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) , Maneno Mbegu (kulia) ambaye anasakata na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta katika hafla iliyoandaliwa na TBL kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma juzi, baada ya wabunge kushiriki bonanza la michezo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment