Wasanii wa kundi la mziki wa kizazi kipya la WISE CREW wamepongezwa na uongozi wa chuo kikuu chaTUMAINI ARUSHA baada ya kuhitimu masomo yao ya shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii pia na juhudi zao za kimuziki zilizosaidia kukitangaza chuo hicho kupitia mziki nasi wadau tunawapongeza kwa kupata hilo jiwe.
Hayo yalisemwa na uongozi wa chuo baada ya wanafunzi hao ambao ni wasanii kuhitimu elimu yao waliyokuwa wakipata chuoni hapo takriban miaka mitatu wakifukuzia shahada ya kwanza ya sayansi ya Jamii nasi FULLSHANGWE tunawapongeza Wise Crew kwa hizo Nondooz mlizopata tunawatakia kila mafanikio katika maisha yenu ya kijamii na ya kimuziki pia.
0 comments:
Post a Comment