Wafanyakazi 70,000 wa ujenzi wa viwanja nchini Afrika Kusini, wameanza mgomo ambao umesitisha kazi muhimu katika taifa hilo kujiandaa kwa michuano ya Kombe la Dunia, mwaka 2010.
Vyama vya wafanyakazi vimetisha kuvuruga michuano hiyo ikiwa madai yao ya kuongezewa mishahara kwa asilimia 13 hayatatimizwa.
Hata hivyo wanaohusika na kuandaa mashindano hayo wanasema wana uhakika kazi katika viwanja hivyo itakamilika, labda tu iwe mgomo utaendelea kwa miezi.
Siku ya Jumatatu mahakimu walikataa malalamiko ya waajiri, kwamba mgomo huo utangazwe sio halali.
Vyama vya wafanyakazi vinaelezea hakuna tarehe iliyotengwa kurudi kazini, na mgomo unaweza kuendelea kwa muda mrefu.
Mwandishi wa BBC, Mpho Lakaje, akiwa Soweto, anaelezea wafanyakazi nje ya uwanja wa Soccer City, na waliovalia magwanda ya kazi, wamekuwa wakitoa vitisho kwa kubeba magongo.
"Tunajitahidi maishani kwa sababu ya nchi yetu", waliimba baada ya kuweka chini vifaa vyao vya kazi.Habari kwa hisani ya mtandao wa http://www.bbcswahili.com/

0 comments:
Post a Comment