WAJASILIAMALI WAPEWA SOMO NA MSOMI WA CHUO KIKUU!!

Mtoa Mada mkuu ambaye ni msomi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es alaam Mlimani anayechukua Phd katika masuala ya Ujasiliamali Bw. Stephano Kingazi akitoa mada mbalimbali kwa washiriki wa semina hiyo juu ya masuala mbalimbali ya ujasiliamali zikiwemmo mbinu mbalimbali katika kukabiliana na changamoto zinazohusu masuala ya unjasiliamali, semina hiyo ya siku moja imefanyika leo kwenye ukumbi wa Ceemi ulioko katika makao makuu ya ofisi za NIMR Ocean Road jijini Dar es alaam
Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo.

Bi Agricola Kossey muandaaji wa semina hiyo naye alipata muda wa kutoa mada kadhaa katika semina hiyo iliyojadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na chanagamoto zinazoweza kuwapata wajasiliamali katika shughuli zao za kibiashara iliyofanyika kwenye ukumbi wa ceemi ofisi za NIMR Ocean Road.
Mkurugenzi wa CarpanyDesign wa pili kutoka kulia Bw. Mathew Lauwo naye alikuwepo katika semina hiyo ili kuona ni jinsi gani anapata mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali katika ujasiliamali.
Mratibu wa semian hiyo Agricola Kossey kushoto akiwa amekaa na washiriki wengine wakimsikiliza kwa makini mtoa mada na Msomi anayechukua Phd katika mambo ya Ujasiliamali katika chuo kikuu cha Dar es alaam Mlimani Bw Stephano Kingazi katika ukumbi wa Ceemi Makao makuu ya ofisi za NIMR Ocean Road.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment