VODACOM YAMWAGA MADAWATI SHULE YA MSINGI UPENDO KONGOWE!!

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Upendo kongowe kata ya Toangoma wilaya ya Temeke Elizabeth Yona(kushoto)akimpa mkono wa shukrani Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya mashariki Atilio Lupara wakati Vodacom Foundation ilipokabidhi madawati 80 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6 kwa shule hiyo ambapo kampuni hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za Msingi za Mkoa wa Dares Salaam.
Afisa Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu akimfunga kamba za viatu mwanafunzi Abdul Wahid wa shule ya Upendo kongowe kata ya Toangoma wilaya ya Temeke ,Vodacom Foundation ilipoenda kutoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6 kwa shule hiyo ambapo kampuni hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za Msingi za Mkoa wa Dares Salaam.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Upendo kongowe kata ya Toangoma wilaya ya Temeke wakipiga makofi kama ishara ya kufurahia msaada waliopokea kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania ambao ni madawati, 80 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6 katika shule hiyo ambapo kampuni hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za Msingi za Mkoa wa Dares Salaam.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment