Mama Salma Kikwete akiwa katika ziara moani Mwanza hapa alikuwa kaizindua ofisi za SACCOS ya Nyalikungu Wilayani Maswa.
Na Anna Nkinda - `Maelezo
Mwanza Shirika la Kikristo la walio katika mstari wa Mbele kupeleka Injili Ulimwenguni (C.L.W.M.F - Christian Life Word Mission Fronties in Tanzania ) linatarajia kujenga Chuo Kikuu cha Kilimo katika wilaya ya Sengerema kuanzia mwaka ujao.
Hayo yamesemwa jana na Rais wa Shirika hilo Mchungaji Pauly Kein wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku sita la kuombea amani Tanzania na kulaani mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yaliyofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
“Leo hii tutasaini makubaliano ya kuanza kwa ujenzi wa Chuo hiki ambao utaanza hapo mwakani ambapo chuo hiki kitaanza kutoa elimu kwa wananchi kuanzia 2012”, alisema.
Mchungaji huyo aliendelea kusema kuwa shirika hilo limekuwa likifanya kazi mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha afya Bukoba, kuwasaidia baadhi ya vijana wasiojiweza kuendeleza masomo yao hadi sasa kuna vijana sita ambao wanawasomesha nje ya nchi.
“Tuna chuo cha kusaidia jinsia ya kike kuongeza kipato ambacho kinafundisha ufundi cherehani huko Bwiru Mwanza pia licha ya kufanya kazi zetu hapa nchini Temecula tukifanya kazi kama hizi za kusaidia jamii katika nchi mbalimbali kama vile Uganda, Rwanda, Burudni na Demokrasia ya Congo ”, alisema Kein.
Akifungua Kongamano hilo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na maendeleo (WAMA) aliwataka wananchi kumkumbuka Mwenyezi Mungu si wakati wa shida peke yake bali hata wakati wa raha pia.
Mama Kikwete alisema, “Serikali yetu haina dini ila wananchi ndiyo tunaabudu katika imani tofauti hivyo basi ni jukumu letu kuheshimu dini ya kila mmoja wetu ili kuilinda amani iliyopo katika nchi hii”.
Kuhusiana na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sengerema Mama Kikwete alilishukuru shirika hilo kwa kuamua kujenga chuo hicho ambacho kitawapatia watanzania elimu.
“Ninaamini kuwa ingawa chuo chenu kitakuwa cha dini ya kikristo pale kikishakamilika na kuanza kazi mtawachukua wanafunzi wa imani zote kama vinavyofanya vyuo vingine vya elimu hapa nchini”, alisema.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alilipongeza Shirika hilo kwa kitendo chake cha kuwapeleka wanawake 27 wa Tanzania nchini Korea ya Kusini kwenda kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo ambao walifanikiwa kufungua mlango wa mahusiano baina ya na wanawake wa nchi hiyo na hivyo wakakubaliana kushirikiana kwa mambo mengi ya kuendeleza jamii zetu.
Kongamano hilo ambalo lilianza tarehe 14 mwezi huu mada mbailmbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na ujane, kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi, yatima, Ukimwi ya ukimbizi.
Mwisho.

0 comments:
Post a Comment